Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, December 10, 2011

Ushirikishwaji duni wa wananchi wakwamisha miradi Kigoma

IMEBAINIKA kuwa kukwama kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ya wananchi vijijini kunatokana na kutokuwepo kwa ushirikishwaji wa jamii wakati wa kuibua na kupanga bajeti ya miradi hiyo.

Mratibu wa Shirika la Uwezeshaji (KIOO), Edward Saimon alisema hayo wakati akisoma

taarifa ya utafiti ya ufuatiliaji wa matumizi ya sekta ya umma uliofanywa katika kata 18 za
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Saimon alisema kuwa utafiti umegundua kuwa sehemu kubwa ya utafiti huo inaonesha

kuwa karibu miradi yote iliyotembelewa kwenye kata hizo ikiwa kwenye Sekta ya Elimu na
Afya ama iliibuliwa na kila kitu kufanywa na kata au wakuu wa idara katika halmashauri.

Aidha ripoti hiyo imeelezea pia kutokuwepo kwa mahusiano na mtiririko unaoeleweka wa

utoaji wa taarifa kutoka katika taasisi za serikali mfano wa shule, zahanati na vituo vya afya
kwenda kwa Mtendaji wa Kata ambaye kwa muundo wa sasa ndiye msimamizi wa mali za
serikali katika kata.

Mratibu wa Shirika la KIOO alisema kuwa imekuwa ni vigumu sana kupatikana kwa taarifa

katika ofisi za watendaji wa kata kuhusu mapato na matumizi ya shule za msingi na sekondari
katika maeneo yao na kwa kiasi kikuwa wakuu wa shule za sekondari wamekuwa wakichangia
hali hiyo.

Hali hiyo pia imelalamikiwa na Diwani wa Kata ya Kagera katika Manispaa ya Kigoma Ujiji,

Damas Rashidi ambaye alisema kuwa wakati mwingine wanavunjika moyo kutokana na
miradi inayotekelezwa kuwa si ile waliyopitisha kwenye Baraza la Madiwani.

Rashidi alisema kuwa wakati mwingine miradi inatekelezwa katika maeneo yao inakuwa chini

ya usimamizi wa moja kwa moja wa wakuu wa idara na diwani kama Mwenyekiti wa Kamati
ya Maendeleo ya Kata asiwe na taarifa ya nini kinachofanyika.

Kwa upande wake Meneja Ruzuku wa Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi ulio chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Frida Lekey alisema asasi zisizo za kiserikali zinalo jukumu kubwa katika kutoa elimu kuhusiana na uwazi na uwajibikaji katika jamii.


Meneja huyo alisema kuwa taasisi za Serikali, ofisi za kata na wananchi hawana budi kuzitumia

asasi zisizo za kiserikali katika kuhakikisha zinatoa elimu kuhusu hali ya upatikanaji wa taarifa za mapato na matumizi ya umma katika taasisi za Serikali katika maeneo yao.

No comments: