Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Friday, October 28, 2011

RC: Miradi iliyo chini ya viwango isimamishwe

MKUU wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya amewataka viongozi na wananchi vijijini kutumia nafasi yao kutumia vikao halali kusimamisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya viwango katika maeneo yao.

Machibya alisema hayo wakati akizindua mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo vijijiji unaosimamiwa na shirila lisilo la

kiserikali la Umoja wa Wawezeshaji Kioo.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Kigoma, John Mongela, Machibya alisema wananchi na viongozi katika ngazi za vijiji wanayo nafasi kubwa ya kusimamia na kuhakikisha miradi inayotekelezwa katika maeneo hayo inakuwa na viwango

vinavyokubaliwa.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema katika baadhi ya maeneo kumekuwa na kasoro katika utekelezaji wa maadili na misingi ya uwazi na uwajibikaji kwa kundi la watu kuamua mambo muhimu ya maendeleo bila kupata ridhaa ya wananchi wa maeneo husika.


Alisema hiyo yote inatokana na kutofanyika kwa vikao vya vijiji na wananchi kukaa mbali na matokeo yake hata miradi inapotekelezwa chini ya viwango huishia kulalamika badala ya kutumia vikao vyao kuchukua hatua.


Awali Mratibu wa Shirika la Uwezeshaji Kioo, Edward Saimon alisema kuwa Sh. milioni 104 zinatarajiwa kutumika katika utekelezaji wa mradi huo utakaofanyika katika kata 18 za halmashauri tatu za wilaya za Mkoa Kigoma.

No comments: