WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameagiza kuanzishwa kwa vituo vya biashara mipakani ili wananchi wafanye biashara halali wajiendeleze kiuchumi na kuongeza pato la taifa kwa kodi na vilevile kukomesha biashara ya magendo.

Pinda alikuwa akizungumza katika Kijiji cha mpakani cha Sirari, kwenye mpaka na Kenya, Wilayani Tarime, Mkoani Mara katika siku yake ya sita ya ziara ya wiki moja ya mkoa huo jana jioni.
Alisema biashara mipakani zinaendeshwa kwa magendo na kupitisha bidhaa kwa “njia za panya” kutokana na kutokuwapo kwa vituo halali vya kufanyia biashara.
“Tuhalalishe biashara mipakani ili kuzuia njia za panya, wafanyabiashara kutoka nchi jirani waje wanunue na sisi tuuze na kununua pia,” alisema.
Alimuagiza mkuu mpya wa Mkoa wa Mara, John Tupa, afanye uchunguzi kwenye mpaka na Kenya na baadaye taarifa yake itaiwezesha Serikali kuamua vituo vya biashara viwe wapi, biashara gani ifanywe na kwa kiwango gani.
Tanzania inapakana Nchi za Kenya, kwa upande wa Kaskazini; Uganda, Rwanda, Burundi, Kaskazini Magharibi, Congo, Magharibi; Zambia Kusini Magharibi na Malawi na Msumbiji, kwa upande wa Kusini.
Hivi sasa hakuna vituo rasmi vya biashara na mara nyingi katika maeneo hayo, biashara ya magendo hushamiri, hasa kwenye mpaka na Kenya.
Mapema wanakijiji wa Sirari waliitaka Serikali kuondoa vizuizi visivyo lazima barabarani ambavyo huendeleza rushwa, kupima viwanja na kuanzishwa kwa kituo cha mabasi.
Waziri Mkuu alisema kwa jinsi Sirari inavyokua kwa haraka, Serikali itafikiria uanzishaji wa Mamlaka ya Mji mdogo ya eneo hilo na hivyo masuala hayo yote yatashughulikiwa baada ya hapo.

No comments:
Post a Comment