Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, September 7, 2011

Mbunge atetea kulima kwenye hifadhi Kigoma


MBUNGE wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR – Mageuzi) amepinga uamuzi wa Serikali
kuwakataza wananchi wa jimbo hilo kuacha kulima na kufanya shughuli mbalimbali katika maeneo ya hifadhi ya misitu ya Kagera Nkanda na Muyowosi wilayani humo.

Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Kasulu, Machali alisema uamuzi huo ni unyanyasaji na kuahidi kupigania usitishwe ili wananchi hao waendelee na shughuli zao katika maeneo hayo.

Alisema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakulima na katika maeneo ya Muyowosi
na Kagera Nkanda na kwamba kukatazwa kuyatumia maeneo hayo kwa sasa kutawakosesha
wananchi hao maeneo ya kilimo ambayo ndiyo msingi mkuu wa kiuchumi kwa familia zao.

Serikali iliwataka wananchi kuacha kulima, kufuga na kufanya shughuli nyingine katika
maeneo hayo hadi kufikia Juni 21.

Lakini Machali aliitaka Serikali kusitisha agizo hilo hadi hapo tume itakapoundwa ili kuchunguza na kuona uhalali na umuhimu wa mahitaji ya eneo hilo kwa wananchi.

“Nimewasiliana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), George Mkuchika ili kusitisha agizo hilo la Serikali na Waziri amefanya hivyo.

 

“Jambo la pili ni kujua mustakabali wa eneo hilo na Waziri amekubali kuleta tume ili kuona
umuhimu wa eneo hilo kuachwa liendelee kutumiwa na wananchi,” alisema Machari.

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa Kasulu Mjini amepinga mpango wa Serikali wa kuwachangisha wazazi chakula kwa ajili ya watoto wanaopaswa kuendelea na masomo
wakati wa jioni.

Alisema kuwa mazingira yaliyopo sasa hayaruhusu wazazi kuchangia katika jambo kwani hata miundombinu ya mahala pa kupikia na kulia chakula hayaruhusu kufanyika kwa jambo hilo.

1 comment:

RAJAB ONE said...

kagera nkanda na muyowosi hayo ndo maeneo (W) kasulu kuna patikana mahindi na maharage kwa wingi, serikali iwaruhusu wananchi wayatumie maeneo hayo ili wapate fulsa ya kuwa na maisha bora na pia wataweza kuwasomesha vijana wao kwa kipato watakacho pata.