Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, September 6, 2011

Kampuni za China zadaiwa kumuuzia Gaddafi silaha

 
MAKAMPUNI ya kutengeneza silaha nchini China yadaiwa kukubaliana kumuuzia kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi shehena ya silaha zenye gharama ya Dola ya Marekani milioni 200.
Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Canada Globe and Mail na la gazeti la Times la mjini New York yariripoti jana kuwa, nyaraka za siri ambazo zilitelekezwa mjini Tripoli nchini Libya zilionyesha makapuni hayo ya China kupitia mazungumzo ya siri yalikubaliana kuiuzia Libya makombora ya masafa marefu, matangi ya makombora pamoja na silaha mbalimbali.
Habari zinasema kuwa, makampuni hayo yameamua kufanya uamuzi huo wa kumuuzia shehena ya silaha Gaddafi mnamo kipindi cha miezi ya mwisho ya utawala wake, ambapo kulikuwa na mazungumzo ya siri ya jinsi ya kusafirisha shehena hiyo kupitia Algeria na Afrika Kusini.
"Tuna ushahidi wa kutosha wa mipango inayoendelea kati ya China na Gaddafi, na tuna nyaraka zote za kuthibitisha ilo,” aliliambia gazeti la Times msemaji wa waasi, Abdulrahman Busin.
Shirika la Habari la Kimataifa la Reuters halikuweza kuthibitiha taarifa hizo za nyaraka hizo zilizopatikanam hata hivyo baadhi ya maofisa waliziwekea mashaka taarifa hizo.
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje nchini China ilisema kuwa, wafuasi wa Gaddafi walikuja nchini humo na kufanya mazungumzo na makampuni ya kutengeneza silaha nchini humo lakini serikali ya China ikupata ufahamisho wowote.
Mazungumzo yagonga mwamba
Mazungumzo yaliyo na azma ya kumpa fursa kiongozi wa Libya, Kanali Gaddafi, kusalimu amri na kuziachia ngome zake zilizosalia yamegonga mwamba.
Kwa mujibu wa msemaji mmoja wa waasi wa Libya, hali hiyo inawawia kuanzisha operesheni yao ya mwisho ya kuuvamia mji uliozingirwa wa Bani Walid.
Habari zinasema kuwa, mazungumzo hayo yalikwama baada ya msemaji wa kiongozi wa Libya, Moussa Ibrahim, kushikilia kuwa waasi hao sharti wajisalimishe kabla ya kuingia mjini humo.
Kwa upande mmoja, waasi wanayadhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini na kwa upande wa pili, Kanali Gaddafi na washirika wake wa karibu wanaoendelea kusakwa wanaungwa mkono na wafuasi wengi wa maeneo ya kusini na katikati ya Libya. Ifahamike kuwa juhudi za waasi hao za  kuunda serikali mpya katika mji wa Tripoli zimeshika kasi.
Habari kutoka katika mji wa Bani Walid zinasema kuwa raia katika mji huo hawawezi kutembea kwa sababu wanahofia kupigwa risasi au kutekwa nyara na kutumiwa kama ngao. Habari zinaendelea kusema wanajeshi watiifu kwa Gadaffi wamewataka wanajeshi hao wa upinzani kutoingia mjini humo huku wakiwa na silaha.
Hata hivyo, Serikali ya mpito nchini humo imesema ina uhakika kuwa mwanawe Gaddafi, Khamis ameuawa. Baraza hilo la kitaifa la mpito (NTC) limesema Khamis aliuawa kwenye mapigano makali karibu na mji mkuu wa Tripoli na kuzikwa karibu na mji wa Bani Walid.


No comments: