Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Tuesday, August 23, 2011

UN yakabidhi miradi ya huduma za jamii Kigoma


UMOJA wa Mataifa (UN) umekabidhi miradi ya huduma iliyokuwa ikitumiwa katika kambi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa uongozi wa Wilaya ya Kigoma.

UN kupitia mpango wa utekelezaji wa pamoja unaofanywa na mashirika yaliyo chini yake, imekabidhi shule ya sekondari ya wasichana na wavulana zilizojengwa kwa ajili ya wakimbizi hao. Imekabidhi pia kituo cha mafunzo ya kilimo kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati wa kilimo kwanza. Miradi hiyo ya elimu na kilimo iliyokabidhiwa, ina thamani ya takribani Sh bilioni moja.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Louise Chamberlain alisema kuwa kutolewa kwa misaada hiyo ya kimaendeleo kwa wananchi wa mkoa Kigoma kunaonesha shukrani kwao kwa kutumia rasilimali ndogo waliyokuwa nayo katika kuhudumia wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu.

Mkuu wa shule ya Sekondari ya Lugufu, Valeria Kitwe alisema kuwa pamoja na msaada mkubwa ambao wameupata kutoka kwa mashirika ya umoja wa mataifa, shule inakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa nyumba za walimu na tatizo sugu la maji safi.

No comments: