WAKIMBIZI wa 94 wa Burundi waliokuwa rumande wakikabiliwa na mashitaka ya uhamiaji haramu kutokana na kutoka kwenye kambi yao bila vibali, wametolewa rumande kinyemela na kurudishwa kambini kitendo ambacho Serikali inachunguza.
Raia hao wa Burundi ambao awali walikuwa wamehifadhiwa katika kambi ya Mtabila wilayani Kasulu, walikamatwa wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma baada ya kutoka kambini bila vibali.
Walifunguliwa mashitaka kama wahamiaji haramu na kuwekwa rumande katika mahabusu ya gereza la Wilaya ya Kasulu kabla ya kutolewa kinyemela hivi karibuni na kurudishwa kambini.
Mkuu wa Wilaya Kasulu Kigoma, Dahn Makanga aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa mwishoni mwa wiki kwamba mpango wa kuwarudisha wakimbizi hao kambini umefanywa kinyume cha utendaji na maadili ya uongozi na kwamba serikali imelaani kitendo hicho.
Makanga ambaye ni Mwenyekiti wa kikosi kazi cha kamati ya ulinzi ya mkoa kilichopewa jukumu la kusimamia mchakato wa kurudishwa nchini mwao wakimbizi wa Burundi, alisema kuwa wamefungua jalada la uchunguzi kwa ajili ya kupeleleza mlolongo mzima wa tukio hilo.
Wakimbizi hao walikamatwa wiki iliyopita wakasomewa mashitaka katika Mahakama ya Wilaya Kasulu ambako dhamana dhidi yao ilifungwa na kutakiwa kukaa mahabusu ili warudishwe mahakamani jana.
Baada ya kutoka mahakamani wakimbizi hao walipelekwa katika mahabusu ya gereza la wilaya Kasulu ambako walikuwa wahifadhiwe hadi jana ili kesi yao iendelee mahakamani.
Hata hivyo katika hali isiyoeleweka, wakimbizi hao 94 ambao walikuwa ni miongoni mwa wakimbizi 158 waliokamatwa walirudishwa kambini Mtabila wakiwa wamepakiwa katika mabasi ya Shirika la kimataifa la World Vision.
Habari za uhakika zinaeleza kuwa mpango huo unadaiwa kuratibiwa na viongozi waandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na kwamba kabla ya kuwarudisha kambini kulikuwa na kikao kati ya Mkuu wa gereza la wilaya Kasulu, watendaji katika mahakama ya wilaya Kasulu na baadhi ya askari waliokuwa wakiwalinda wakimbizi hao.
Mkuu wa makazi wa Idara ya wakimbizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani wilayani Kasulu, Frederick Nisajile alisema kuwa kitendo hicho cha kurudishwa kambini kwa wakimbizi hao ni udhalilishaji wa mamlaka na madaraka ya serikali.
Nisajile alisema, jambo la kwanza ambalo anatarajia kulifanya ni kuzuia kuingia kambini kwa madereva wa magari ya World Vision yanayodaiwa kubeba wakimbizi hao.
Alisema, anatarajia kumzuia kuingia kwenye kambi zote za wakimbizi Ofisa Usalama wa UNHCR wilayani Kasulu, akimtuhumu kufanya vitendo vinavyokiuka mipaka yake ya kiutendaji.

No comments:
Post a Comment