MFANYABIASHARA mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Regina
Alphonce (27) amefikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la kumjeruhi kwa
kumchoma moto mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka saba.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Athumani Mshana alidai
mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, David Ngunyale kuwa mshitakiwa
alimchoma kwa moto na kumsababishia maumivu mtoto huyo, ambaye ni mtoto wa
mumewe aliyezaa na mwanamke mwingine.
Mwendesha Mashitaka alidai mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Februari 20
na 23 mwaka huu saa 4 asubuhi katika eneo la Katubuka. Mtoto huyo ni mwanafunzi
wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kiezya iliyopo Manispaa ya Kigoma/
Ujiji.
Mshitakiwa alikana kosa hilo na kudai kuwa ni utundu wa mtoto huyo.
Hakimu Ngunyale aliahirisha kesi hiyo na kuamuru mshitakiwa arudishwe rumande
hadi Machi 14 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.
No comments:
Post a Comment