SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) kwa kushirikiana
na Shirika la Tools for Self Reliance (TFSR) la Uingereza, wametoa vifaa vya
ufundi kwa wajasiriamali wadogo mjini Kigoma kuwawezesha kukuza na kuboresha
shughuli za biashara.
Meneja wa Sido mkoani Kigoma, Gervas Ntahamba alisema kuwa
biashara za wajasiriamali wadogo mkoani humo zimekuwa zikizorota kutokana na
mitaji midogo na uzalishaji usiozingatia viwango vya ubora, kutokana na
matumizi ya vifaa duni vya kuzalishia bidhaa zao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo alisema
kuwa msaada huo unatokana na uhusiano mzuri kati ya Sido na shirika hilo la Uingereza kwa
lengo la kuwakwamua wajasiriamali wadogo.
Ntahamba alisema wajasiriamali wamepewa mafunzo ya mbinu za
kibiashara na utafutaji masoko ya bidhaa wanazozalisha. Vifaa vilivyotolewa ni
vyerehani, vifaa vya ufundi seremala na uhunzi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Alfred Luanda
aliwataka wajasiriamali hao kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili
vilete tija na kuwakwamua kutoka hatua waliyopo.
No comments:
Post a Comment