Miss Kigoma 2012 Anna Willboad (aliyeketi) akiwa na Mshindi wa pili ni Suzan Gregory (wa pili kulia) na mshindi wa watu, Justina Philipo baada ya kutwaa taji hilo juzi.Kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Lilian Mbaga.
MWANADADA Anna
Wilbroad juzi usiku alifanikiwa kunyakua taji la mnyange wa Kigoma kwa mwaka
2012 baada ya kuwashinda washiriki wenzake saba walioshiriki kinyang’anyiro
hicho.
Akitangaza
matokeo ya ushindi, jaji mkuu wa mashindano hayo Rashidi Michumino kutoka ofisi
ya mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, alisema kuwa pamoja na kunyakua taji
hilo mnyange huyo pia amepata zawadi ya fedha Sh 300,000 na kushiriki katika
mashindano ya kanda mkoani Dodoma.
Pamoja na
zawadi hizo pia mshindi huyo amepata zawadi ya kusoma kozi ya masomo ya utalii
kwa mwaka mmoja katika chuo cha Western Tanganyika cha mjini Kigoma.
Mshindi wa
pili katika shindano hilo alikuwa mrembo Susan Gregory aliyepata zawadi ya Sh
200,000, kozi ya masomo ya utalii kwa mwaka mmoja akipata nafasi pia ya
kushiriki mashindano ya ngazi ya kanda mkoani Dodoma.
Jaji wa
shindano alimtangaza mwanadada Justina Philipo kuwa mshindi wa tatu ambaye
alipata zawadi ya fedha taslim Sh 100,000, kozi ya computer, pia akapata nafasi
ya kushiriki katika mashindano ngazi ya Kanda.
Mwanadada
Mwamvita Juma aliibuka kuwa mshindi katika shindano la vipaji na ubunifu ambapo
alizawadiwa Sh 50,000 katika shindano ambalo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya wilaya Kigoma, Lilian Mbaga alikuwa mgeni rasmi.
Akikabidhi zawadi kwa washindi Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya wilaya
Kigoma alitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu
watoto wao kushiriki shindano hilo ambalo kwa sasa limekuwa pia chanzo cha ajira
kwa wasichana wanaofanya vizuri na wenye vipaji.
No comments:
Post a Comment