KIPIMO cha haraka cha kutambua malaria kimeelezewa kuwa
kitasaidia kudhibiti matumizi ya dawa ambazo zilikuwa zikitolewa kwa watu
waliokuwa wakidhaniwa wana ugonjwa huo wakati hawana kutokana na kutokuwepo na
vipimo.
Mganga Mkuu wa Wilaya Kigoma, Edwin Kilimba alisema hayo
wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa zahanati na vituo vya afya
vya wilaya hiyo juu ya matumizi ya kipimo hicho yanayofanyika mjini hapa.
Kilimba alisema kipimo kitasaidia kufahamu kwa uhakika kama
mgonjwa aliyefika kwenye kituo cha afya ana malaria au la
Alisema sehemu kubwa ya zahanati katika wilaya hiyo hazina
darubini ya kupimia malaria na hivyo watoa huduma hutumia mazoea kwa kuangalia
dalili za ugonjwa huo na hivyo kufanya matumizi makubwa ya dawa ya Alu ambayo
hulalamikiwa kwamba huwa zinachukua muda mfupi kuwepo kwenye zahanati.
Mwezeshaji wa mafunzo ya matumizi ya kifaa hicho kutoka
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Matilda Joseph alisema dawa za Alu zimekuwa
na matumizi makubwa nchini kutokana na utoaji holela ikidhaniwa kuwa kila
anayelalamikia maumivu ana malaria
No comments:
Post a Comment