WATU watatu wakiwamo wanafunzi wawili wa shule ya msingi
wilayani Kasulu na mkulima mmoja katika wilaya hiyo, wamefariki dunia kutokana
na kupigwa na radi ambayo pia imejeruhi mtu mwingine.
Akizungumza mjini hapa na waandishi wa habari, Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Fraiser Kashai aliwataja watu hao waliofariki kuwa ni
Jackline Leonald mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Rusesa
wilayani Kasulu na ndugu yake, Maria Leonald walikutwa na mauti wakiwa njiani
kurejea nyumbani wakitokea shambani.
Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefariki katika
tukio hilo kuwa
ni Zuwena Cosmas wa Shule ya Msingi Kagera Nkanda ambapo pia radi hiyo
ilimjeruhi Rahel Lucas (10) mkazi wa kijiji hicho cha Kagera Nkanda ambaye
anapatiwa matibabu kwenye zahanati hiyo ya kijiji.
Kamanda Kashai alisema matukio hayo yaliyotokea saa nne
asubuhi , yanatokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika maeneo hayo
ambayo iliambatana na radi kubwa.
Katika tukio lingine, mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) Mkoa wa Kigoma, Ally Mgaya amejeruhiwa kichwani kutokana na basi
la abiria la Kimotco lililokuwa likifanya safari ya kutoka Kigoma kwenda Dar es
Salaam kupinduka na ambapo abiria zaidi ya 20 walijeruhiwa.
Kamanda Kashai alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Senga
Gungu mjini Kigoma saa 12 asubuhi wakati basi hilo lenye namba za usajili T369 ASE aina ya
Scania lililokuwa likiendeshwa na Mohamed Bakari lilipoacha njia na kugonga
ukuta wa mtaro na kisha kutumbukia mtaroni.
Alisema baada ya ajali hiyo majeruhi hao walipatiwa matibabu
na kuruhusiwa kurudi nyumbani ambapo abiria watatu wamelazwa hospitalini pamoja
na askari
No comments:
Post a Comment