Hotel ya Jimbo Katoriki ya Nzimano Kigoma.
MZIMU wa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, bado unakitafuta chama
cha NCCRMageuzi baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu wa Jimbo hilo,
kushindwa kufanyika kutokana na vurugu kubwa iliyozuka kabla.
Sababu kubwa ya vurugu hiyo ni baadhi ya viongozi wa jimbo hilo, wakiongozwa na Katibu wa Jimbo, Faida Masudi, kutaka baadhi ya wajumbe kutohudhuria mkutano huo kwa kilichoelezwa kuwa si wajumbe halali wa kikao.
Waandishi wa habari ambao walipiga kambi nje ya ukumbi wa Nzimano ambako mkutano huo ulikuwa ukifanyika, walisubiri kwa zaidi ya saa sita kuhudhuria ufunguzi wa mkutano kwa mujibu wa mwaliko wa uongozi wa chama hicho.
Vurugu hizo zilifanyika kabla ya mkutano kufunguliwa kutokana na malumbano ya kutaka kufanyika kwa uhakiki wa wajumbe, yaliyoanza saa nne asubuhi hadi saa 10 jioni na wajumbe kuanza kurushiana makonde.
Hata hivyo, hakuna madhara yaliyotokea kwa wajumbe baada ya polisi zaidi ya sita waliokuwa nje ya ukumbi huo, kuingilia kati na mbali na michubuko midogo waliyopata wajumbe, Masudi alijeruhiwa juu ya jicho la kushoto.
Akizungumza na waandishi wa habari, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR - Mageuzi kutoka Mkoa Kagera ambaye alikuwa afungue mkutano huo, Peterson Mshenyera, alisema mkutano ulishindwa kufanyika kutokana na vurugu za wajumbe wakati wa uhakiki wa wajumbe halali wa mkutano.

No comments:
Post a Comment