MAMLAKA ya Mapato(TRA) mkoani Kigoma, imedai kuwa utendaji duni wa
Kampuni ya Reli (TRL) na miundombinu duni ya barabara kuingia na kutoka
mkoani Kigoma ni moja ya changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo katika
kufikia malengo ya ukusanyaji mapato iliyojiwekea.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Meneja wa TRA wa Mkoa Kigoma, Ernest Dundee, Ofisa Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi, Sixmond Kafuru alisema kuwa hali hiyo inafanya kutokuwepo kwa mzunguko mkubwa katika kuuza na kununua bidhaa mkoani humo.
Sambamba na changamoto hizo, alizitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ukwepaji kodi wa bidhaa kutoka nje ya nchi, vyanzo vichache vya mapato huku sehemu kubwa ya vyanzo hivyo ikitegemea ridhaa ndogo ya ulipaji wa hiari kutoka kwa wananchi.
Kafuru alisema inailazimu TRA wakati mwingine kutumia fedha nyingi na nguvu za ziada kuwafuatilia wafanyabiashara ili walipe kodi zao kwa wakati. Alisema kuwa tatizo la wafanyabiashara kutokuwa na utunzaji sahihi wa kumbukumbu za biashara na kutotoa risiti kwa bidhaa zinazouzwa bado ni changamoto kubwa inayowakabili.
Mkakati uliopo wa kukabiliana na changamoto hiyo kwa mujibu wa Kafuru, ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili waone umuhimu na faida ya kulipa kodi zao kwa hiari na kwa wakati.
Akizungumzia hali ya ukusanyaji mapato, Kafuru alisema kuwa mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3.1 katika kipindi cha nusu mwaka kwa mwaka huu wa fedha.
Makusanyo hayo ni sawa asilimia 94 ya lengo la kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3.2 kwa kipindi hicho.
Aidha Kafuru alisema kwa mwaka huu wa fedha, makusanyo hayo yamepanda kwa kiasi cha Sh milioni 468.9 ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 na kwamba hilo linatokana na uimarishaji wa vitalu vya uwindaji na elimu kwa walipa kodi.

No comments:
Post a Comment