BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya wilaya Kigoma limeazimia kusitishwa
kwa utafiti wa madini unaofanywa katika eneo la Kaparaguru, Kata ya
Igalula wilaya ya Kigoma kutokana na halmashauri kutokuwa na taarifa
yoyote ya kinachofanyika mahali hapo kwa miaka 50 sasa.
Akitoa hitimisho la azimio hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Hamisi Betese alisema kuwa kwa muda mrefu halmashauri hainufaiki kwa lolote na kinachofanyika mahali hapo na kueleza kuwa wanachoona ni wizi wa madini ndiyo unaoendelea.
Betese alisema kuwa kwa muda mrefu sasa makampuni ya kigeni yamekuwa yakifanya utafiti, lakini watu mbalimbali wameshuhudia uchimbaji unaoendelea na malori yakibeba mchanga kutoka sehemu hiyo lakini kila wanapouliza taarifa unasema kwamba kinachofanyika ni utafiti.
Zaidi ya hilo, alisema kuwa wameyaandikia barua makampuni yanayofanya utafiti huo kufika ofisini kwao na kutoa maelezo ya nini kinafanyika, lakini viongozi wa makampuni hayo wamekuwa wakaidi.
Mwenyekiti huyo wa halmashauri alieleza kuwa ni jambo lisilo eleweka kuona kampuni inafanya uwekezaji mkubwa, ikiwa ni pamoja na kujenga kiwanja cha ndege, barabara za kuingia eneo hilo na majumba ya thamani kubwa mahali hapo lakini kila wanapoulizia wanaambiwa ni utafiti tu unaofanyika.
Wakiunga mkono azimio hilo madiwani hao walisema kuwa wamechoshwa na wizi wa madini unaoendelea katika eneo hilo huku halmashauri ikiwa hainufaiki kwa lolote ambalo linafanyika mahali hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kigoma, John Mongela alisema kuwa ni kweli kumekuwa na utata wa kile kinachofanyika mahali hapo kwa muda wote huo na kabla ya kuchukua hatua yoyote ameliomba baraza kuiandikia ofisi ya Ofisa Madini Mkazi Mkoa wa Kigoma kupata ufafanuzi wa jambo hilo.
Mongela alisema kuwa anachojua ni kwamba pamoja na makampuni ya uchimbaji yaliyopo eneo hilo, lakini pia ipo taasisi ya serikali ambayo inaliangalia jambo hilo kwa karibu na kwamba busara itumike katika kufikia suluhu ya jambo hilo.
Akizungumzia kuhusu utafiti unaofanywa katika eneo hilo, Ofisa Madini Mkazi mkoa Kigoma, Adam Juma alisema kuwa utafiti wa kwanza ulifanyika kuanzia mwaka 1930 na kampuni yaa Kijerumani ambapo ramani za kijiolojia zilitengenezwa.
Kwa sasa kampuni ya Nyati Mining (T) kwa kushirikiana na kampuni ya Gold Stream na IAM Resources ya Australia ndiyo inayoendelea na utafiti katika eneo hilo sambamba na taasisi ya Serikali ya Geological Survey Tanzania (GST).
Hata hivyo alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 2010 kampuni inaruhusiwa kufanya utafiti katika eneo moja kwa muda usiozidi miaka tisa na kwamba yapo makampuni mbalimbali yalifanya utafiti eneo hilo na kuondoka.

No comments:
Post a Comment