MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jenerali Simon Kitundu amesema
kuwa Jeshi hilo halikuundwa kwamadhumuni ya kuwatafutia vijana kazi,
bali kuwaanda wajitegemee na kumudu maisha yao baada ya kumaliza
mafunzo.
Alisema hayo jana katika Kambi ya JKT Bulombora kikosi cha 821, katika kilele cha maadhimisho yakufunga mafunzo ya vijana ya Operesheni Miaka 50 ya Uhuru.
Jenerali Kitundu alisema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Ofisa Utumishi Mkuu wa JKT, Luteni Kanali Eslom Lubinga na kuwataka vijana wanaotaka
kujiunga na JKT kuondoa dhana ya kupata ajira kutoka katika jeshi hilo.
Alisema kuwa JKT ni kama chuo kama ilivyo vyuo vingine vya ufundi stadi na kinatoa elimu ya kujitegemea ili watumie mafunzo waliyopata kulitumikia Taifa.
Alisema kuwa JKT kwa sasa inatumika kama sehemu ya kuwaandaa vijana kujiunga na majeshi mbalimbali nchini ikiwemo Polisi, Magereza, Uhamiaji na Usalama wa Taifa kwa wale wenye sifa.
Jenerali Kitundu pia aliitaka Serikali kuitumia JKT kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa miradi mbalimbali ili kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi hiyo lakini pia kuifanya miradi hiyo kukamilika kwa haraka.
Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya alisema kuwa mafunzo ya JKT yanalenga kuwafanya vijana waliopitia mafunzo hayo kuwa sehemu ya Jeshi la akiba la nchi hii na tayari kutumika itakapobidi kufanya hivyo.
Machibya alisema kuwa JKT imekuwa chuo kinachowapika vijana kuwa na uzalendo kwa nchi yao, ujuzi wa kazi za mikono na kujua hali ya nchi yao ilivyo na hivyo kujituma kwa kiwango cha hali ya juu katika utendaji wao.
Alisema kuwa kuondolewa kwa mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria kuliondoa yote hayo na matokeo yake kumekuwa na migomo katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.

No comments:
Post a Comment