Kabwe Zitto
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Kabwe Zitto amepongeza Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya
kiwango cha lami kutoka Kigoma hadi Uvinza na kukamilika kwa Daraja la
Malagarasi.
Zitto alitoa pongezi hizo kwenye mkutano wa hadhara wa chama
chake uliofanyika mjini Tabora.
Pia, katika mkutano huo, aliwahimiza wananchi wa Tabora
kupata mbunge kutoka Chadema, kwa kile alichodai kuwa bila kufanya hivyo,
hawatapata barabara za lami.
Alisema barabara ya kutoka Uvinza kwenda Tarafa ya Nguruka,
Kigoma Vijijini inaendelea kukamilishwa kwa kiwango cha lami ili wananchi wa
Kigoma waendelee kutumia kodi yao
kikamilifu.
Alisema licha ya hayo yote, Serikali bado ina wajibu mkubwa
kuhakikisha wananchi wa Tabora, pia wananufaika na miradi ya barabara kwa
kiwango cha lami. Zitto alisema alipita njia ya kutoka Kigoma hadi Tabora Mjini
kupitia Nguruka na Urambo na kujionea barabara ilivyo mbovu.
Alisema tatizo kubwa lililopo ni kuunganisha barabara hizo
na mikoa mingine nchini.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema jambo
linalomkera ni uwepo wa utitiri wa vyama vingi nchini, ambavyo alidai vingi
havijui mustakabali wa nchi.
Alisema utitiri huo, unasababisha upinzani kushindwa
kukamata Dola na kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment