MWANAFUNZI wa Chuo cha Ualimu Kigoma, Valerian Nicodemus
(22) ameshinda Sh milioni 100 za promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom.
Nicodemus ameibuka mshindi wa jumla wa promosheni hiyo baada
ya kuchezeshwa kwa droo kubwa iliyoshirikisha mamilioni ya washiriki, ambao ni
wateja wa kampuni hiyo ya simu.
Akizungumzia ushindi, Nicodemus alisema hakutarajia maishani
mwake kupata kiasi kikubwa cha fedha kama
hicho.
Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa moja katika Promosheni
hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na Mzee niliamua kuweka na kushiriki
katika Promosheni hii, hakika nimefurahi sana
na ninawashukuru Vodacom,” alisema.
Aliendelea kusema, “Awali sikuwa naamini kabisa kama kweli mtu anaweza kushinda kihalali, yalikuwa mawazo
potofu, lakini kweli yametokea na ninamshukuru Mungu na pia Vodacom kwa kuyabadilisha
kabisa maisha yangu”.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,
Kelvin Twissa amempongeza Nicodemus na washindi wengine.
Alisema anajivunia mafanikio ambayo promosheni hiyo
imeyapata kwa kubadili maisha ya mamia ya Watanzania.
Tangu kuanza kwa promosheni hiyo Januari 24 mwaka huu,
washindi 333 wamepatikana na kugawana zaidi ya Sh milioni 480 zilizokuwa
zinashindaniwa na washindi kupatikana kila siku, kwa wiki na hatimaye droo kubwa
iliyompa ushindi Nicodemus.
No comments:
Post a Comment