MAHARAMIA kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) waliovamia
wavuvi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika na kukabiliana na polisi na
wanajeshi kwa saa nane wamezamishwa ziwani, imethibitishwa.
Uthibitisho huo umetolewa baada ya boti yao kushambuliwa kwa silaha nzito na vikosi vya ulinzi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Fraiser Kashai, alithibitisha hilo jana mbele ya waandishi wa habari, baada ya jambo hilo kutozungumzwa kwa siku tatu.
Alisema kuzamishwa kwa maharamia hao ambao idadi yao haikujulikana kunatokana na kubainika kutumia silaha nzito zikiwamo bunduki za masafa marefu-RPG. Pamoja na kuthibitishwa kuzamishwa kwa boti hiyo, Kamanda Kashai hakueleza kama maharamia hao waliuawa au la.
Lakini habari za uhakika zinaeleza kuwa maharamia hao waliuawa kwa mizinga mizito ya kutungulia ndege, iliyotumiwa na vikosi vya Tanzania katika mashambulizi hayo.
Sambamba na kuzamishwa kwa boti hiyo, Kamanda alisema pia boti ya Polisi na askari wa JWTZ ilizamishwa ikiwa na wapiganaji wanane ambao hata hivyo waliokolewa baada ya kuelea majini kwa saa kadhaa.
Alisema miongoni mwa waliookolewa ni pamoja na Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai wa Wilaya ya Kigoma, Mohammed Kilonzo, ambaye alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi kifuani.
Katika tukio hilo, Kamanda Kashai alisema polisi konstebo, aliyejulikana kwa jina la Kumalija, aliuawa kwa risasi zilizomjeruhi Kilonzo.
Pamoja nao alisema pia wanajeshi wanne wa JWTZ kutoka kikosi cha 24KJ Kigoma walijeruhiwa, na ambao ni Kombo Ame Basha, Juma Dadi, Emmanuel Kimaro na Hassan ambapo majeruhi wote walipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Akieleza chanzo cha mapigano hayo, Kamanda Kashai alisema saa nane usiku wa kuamkia Mei 3 Ziwa Tanganyika eneo la Msalabani, maharamia kutoka DRC walivamia wavuvi na kuwanyang'anya injini za boti na vifaa mbalimbali na kurejea tena saa 11 alfajiri na kuteka injini zingine na vifaa vyote vikiwa na thamani ya jumla ya Sh milioni 14.
Baada ya mashambulizi hayo Kamanda alisema vikosi vya JWTZ kikosi cha 24 na polisi wanamaji viliendelea kufanya doria ndani ya Ziwa.

No comments:
Post a Comment