Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Thursday, September 13, 2012

I Missing a lot this beautiful place

Kigoma mjini (LEKA DUTIGITE)

Wednesday, September 12, 2012

POLISI KIGOMA WAOKOA WATATU WANAOTUHUMIWA KWA UCHAWI

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SSP Joseph Konyo


Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa, wa Polisi Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa kuwaokoa watu watatu waliokuwa
wamezingirwa na kundi la wananchi wakitaka kuwaua kwa tuhuma za
kujihusisha na vitendo vya ushirikina.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SSP Joseph Konyo, aliwataja watu hao
waliokolewa kuwa ni Evania Sephanga(50), mkazi wa wilaya ya Kibondo,
Bruno January(46), mkazi wa kijiji cha Nyamhoza na mtoto mmoja mwenye
umri wa miaka kumi na mkazi wa kijiji cha Nyamhoza Kigoma mjini ambaye
jina lake linahifadhiwa.

Kamanda Konyo amesema kuwa wiki iliyopita majira ya saa tisa mchana, watu hao
walizingirwa na kundi hilo kwa madai kuwa walimroga na kumuua msichana
mmoja aitwaye Faines Zawadi(20) mkazi wa kijiji hicho cha Nyamhoza
ambaye siku moja kabla ya kifo chake alionekana kama mtu
aliyechanganyikiwa na kuwa kama kichaa.

Alisema katika tukio hilo, bibi kizee mmoja ambaye alikuwa mshirika wa kundi la
waliodaiwa kuwa wachawi, alifanikiwa kutoroka katika mazingira ya
kutatanisha alipojifanya kuwa anakwenda kujisaidia.

Kamanda Konyo amemtaja bibi huyo aliyefanikiwa kutoroka kuwa ni Bibi Editha
Dosiyo mkazi wa kijiji hicho ambaye baadaye alipatikana na kuhojiwa
kabla ya kukabidhiwa kwa Idara ya ustawi wa jamii baada ya kuonekana
kuwa maisha yake yangekuwa hatarini.

Amesema baada ya Polisi kupata taarifa za tukio hilo, walikimbia na kwenda
kuwaokoa kutoka katika mikono ya kundi la wananchi lakini wakiwa
wameshaadhibu ingawa ilikuwa haijawa kwa kiasi kikubwa.

Habari zinasema kuwa, baadhi ya wananchi walipata taarifa kutoka kwa mtoto
aliyeokolewa akisema kuwa baadhi ya watoto waliofariki kijijini hapo,
akiwataja (majina tunayahifadhi) alikuwa akiwaona nyumbani kwao nyakati
za usiku wakiosha vyombo na baadaye kupewa chakula.

Siku ya tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema kuwa kabla ya bibi huyo
kutoweka alimnong’oneza jambo mjukuu wake ili amfanyie mareheme ikiwa ni
pamoja na kumruka mara saba kisha bibi huyo alitoweka akijifanya
anakwenda kujisaidia.

Walisema mara baada ya bibi huyo kutoweka, mtoto huyo wa kiume ambaye ni
miongoni mwa waliozingirwa wakitaka kuuawa, aliamza kutekeleza maagizo
ya bibi huyo na alipomaliza kitendo cha kumruka kwa mara ya saba,
msichana yuyo ambaye alikuwa ni marehemu alizinduka na kuomba uji.
Wamesema msichana huyo ambaye alikuwa mfu, alipewa uji na kunywa kisha
akapelekwa hospitalini ambako hadi sasa hali yake inasemekana kuwa
inaendelea vizuri.

Hata hivyo Kamanda Konyo ametoa wito kwa wananchi kuacha kuchukua sheria
mkononi na badala yake watoe taarifa Polisi kwa kila jambo wanaloliona
kuwa linaweza kuleta uvunjifu wa amani ili hatua za haraka zichukuliwe
dhidi ya wahusika.

Mwezi uliopita watu wawili mke na mume, waliuawa na kundi la watu wenye 
hasira kisha miili yao kuchomwa kwa moto mkoani Kigoma baada wa 
kutuhumiwa kuwa walikuwa ni wachawi.

AKAMATWA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA BINADAMU

MKAZI wa Kijiji cha Kitema, Kata ya Nyakitonto, Yolam Venance (26), anashikiliwa na Idara ya Uhamiaji wilayani Kibondo mkoani Kigoma, kwa kosa la kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu kutoka Burundi na kuwaingiza nchini kinyume na sheria.

Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Kibondo, Njunwa Mlaki, alisema walimkamta akiwasafirisha vijana saba wenye umri wa chini ya miaka 17 kutoka Burundi akiwapeleka wilayani Kasulu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi ya kuchunga ng’ombe.

Aliwataja watoto hao waliokuwa wakisafirishwa kuwa ni Ngarukiye Fransis (16), Niyonkuru Erick (16), Nsimilimana Erick (11), Mubaimana Lamek (15), Sibomana Janemarie (15), Tivugwa Bimenyimana (15) na Imani Tharawis (11).

Baada ya vijana hao kukamatwa, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto akiwa ameambatana na maofisa uhamiaji wamewasafirisha vijana hao hadi mpakani mwa Burundi na Tanzania na kuwakabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Gisuru nchini Burundi, Ndikuliyo Egide, kwa ajili ya kuwarudisha nyumbani kwao.

Alisema idara yake ilipata taarifa kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili wakati wowote ushahidi utakapokamilika.

Alisema Watanzania wanoishi mikoa ya mipakani hasa Kigoma na Kagera wanapenda kutumia nguvu kazi ya watu hasa kutoka Rwanda na Burundi kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Aliwataka Watanzania kufuata sheria na taratibu za uhamiaji za nchi na haki za binadamu wanapokuwa wanawaingiza watu nchini kutoka nchi mbalimbali.