TIMU ya Ruvuma imeanza vema mashindano ya Copa Coca-Cola
yanayoshirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17 ngazi ya Taifa baada ya
kuwalaza mabingwa watetezi Kigoma mabao 2-0 katika mchezo wa kundi A
uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar
es Salaam.
Kigoma ambao walianza mashindano kwa kasi na kuwatandika
Lindi mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi mwishoni mwa wiki iliyopita, jana
walishindwa kufurukuta mbele ya Ruvuma na
kuruhusu bao katika kila kipindi.
Mabao yote ya washindi yalifungwa na mshambuliaji Edward
Songo katika dakika ya 34 na 84. Katika mechi nyingine za jana, Tanga na
Morogoro walitoka sare ya mabao 3-3 kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Tanganyika
Packers, Kawe jijini.
Mkoani Pwani, Mara waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Temeke Uwanja wa Nyumbu, wakati Kagera walilala kwa bao 1-0 mbele ya
Kilimanjaro katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Tamco.
Wakati huohuo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza
dau kwa wapigapicha za magazeti watakaoripoti mashindano ya Copa Coca-Cola
yanayoendelea kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola na
kushirikisha mikoa 28 yanafanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kumbukumbu ya
Karume mkoani Dar es Salaam, na Viwanja vya Tamco na Nyumbu mkoani Pwani.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Mwabura alithibitisha taarifa
hizo na kusema zawadi ya Sh 250,000 itatolewa kwa picha bora katika maeneo
matatu.
Aliyataja maeneo hayo kuwa ni picha ya kitendo (action
picture), haki (fair play picture) na mpigapicha ambaye ameripoti matukio mengi
ya mashindano
No comments:
Post a Comment