Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Luteni kanali mstaafu Issa Machibya
Wakuu
wa wilaya mbalimbali mkoani Kigoma wamekula viapo vya utii na kuahidi
kushirikiana na wananchi katika kusimamia kikamilifu maswala ya ulinzi
na usalama, utekelezaji wa miundo mbinu ya huduma za jamii zikiwamo za
elimu, afya na utekelezaji wa miradi ya kilimo na uvuvi.
Wakuu
hao wa wilaya sita tofauti, wametoa ahadi hizo kwa nyakati tofauti
baada ya kula kiapo cha utumishi wao mbele ya mkuu wa mkoa wa Kigoma
Luteni kanali mstaafu Issa Machibya.
Waliokula
kiapo cha utii wa utumishi ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Kasulu Dany
Makanga ambaye kabla ya kuhamishiwa kituo kipya cha kazi alikuwa ni mkuu
wa wilaya ya Kibondo na amekuwa akikaimu wilaya za Buhigwe, Kakonko na
Kasulu yenyewe.
Wengine
waliokula kiapo cha utii ni pamoja na mkuu wa wilaya mpya ya Uvinza
Hadijah Nyembo, Venance Mwamoto ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kibondo na
Gishule Charles ambaye atakuwa katika wilaya mpya ya Buhigwe.
Kanali
Cosmas Kayombo yeye amekula kiapo cha kuwatumikia wananchi wa wilaya
mpya ya Kakonko, wakati Rajabu Maneno ameapa kuwa mkuu wa wilaya ya
Kigoma.
No comments:
Post a Comment