Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya
MKUU wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya amepiga marufuku kwa
wakulima mkoani humo kuuza kahawa kwenye madebe.
Aidha amewaagiza wakulima hao kutoanika kahawa yao chini kwani kwa kufanya hivyo wanaiondolea ubora kwenye soko la dunia. Machibya alitoa maagizo hayo kutokana na michango mbalimbali iliyotolewa na wadau wa kahawa mkoani humo inayoonesha kuwa kutosimamiwa kwa sheria za uzalishaji wa zao hilo kumechangia kushusha ubora wa zao hilo.
Mkuu huyo wa mkoa alizitaka halmashauri za mkoa huo kwa kutumia mabaraza yao ya madiwani kutunga sheria ndogo za kusimamia zao hilo.
Alisema kuwa taarifa zinaonesha kuwa kahawa inayozalishwa mkoani Kigoma imekuwa ikipendwa maeneo mbalimbali duniani na wanunuzi wamekuwa wakiikimbilia lakini uzalishaji usiozingatia viwango vya ubora unachangia kuwakimbiza wanunuzi hao.
“Kwa sasa serikali ya mkoa itajiingiza kikamilifu kuhakikisha inasimamia kwa karibu uzalishaji unaozingatia ubora wa juu wa zao la kahawa mkoani Kigoma na hatutakubali kuona mtu mmoja anaturudisha nyuma katika hilo kwa kile kitakachotokea,” alisema .
Awali Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Kahawa mkoani Kigoma (KANYOVU), Jeremia Nkangaza alisema kulegalega kwa sheria za usimamizi na uendelezaji wa zao hilo, k
Nkangaza alisema kumekuwepo mkanganyiko katika namna ya kushughulikia mifumo ya masoko ya kahawa mkoani humo lakini akaonya kuwa hakuna mnunuzi yeyote ambaye yuko tayari kununua kahawa isiyo na ubora.
Meneja wa Bodi ya Kahawa (TCB) mkoani Kigoma, Kaberwa Rutachweka alisema kuwa masoko ya kahawa yapo wakati wote hata kama wakati mwingine bei inakuwa imeshuka kwenye soko la dunia lakini kahawa yenye ubora wa juu haiwezi kukosa wanunuzi. umechangia kushusha ubora wa zao hilo kwa msimu huu hali iliyosababisha wakulima kupata bei ya chini katika soko la dunia.

No comments:
Post a Comment