Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Wednesday, April 11, 2012

Sh17 milioni zakusanywa Kigoma

Luteni  Kanali  Mstaafu Issa Machibya 

ZAIDI ya Sh17 milioni  zimekusanywa  katika harambee iliyoendeshwa na  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,  Luteni  Kanali  Mstaafu Issa Machibya kwa lengo la kujenga Shule ya Sekondari ya elimu ya juu ya mkoa .

Katika harambee hiyo,  fedha taslimu Sh6.5 milioni  zikusanywa huku wadau wengine wakitoa ahadi ili kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika na kuondoa kero ya uhaba wa shule za sekondari.

Hayo yamesemwa na Machibya wakati wa Kikao cha Baraza la Ushauri cha Mkoa wa Kigoma ,  na kutaka harambee hiyo kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau wa elimu walio na uzalendo katika ngazi ya kitaifa.

Alisema lengo la mkoa haliishii katika harakati za kujenga  sekondari pekee , bali wanatarajiwa kupata Chuo Kikuu  ili wakazi wa mkoa huo waondokane na changamoto za   ujinga na  umaskini  kwa  kupata wataalam ambao ni wazawa wa mkoa huu.

Aidha aliwataka viongozi wa vyuo mbalimbali mkoani hapa,  kuongeza wigo wa kitaaluma ili kuendana na soko la wawekezaji kwa siku zijazo na kwamba vijana ambao ni wazawa watapata ajira katika viwanda na makampuni mbalimbali na kuondoa wimbi la uzururaji.

Kwa upande wake  Katibu wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Msafiri Wamarwa  alipongeza hatua hiyo na kusema utekelezaji huo ufanyike kama ilivyo pangwa .

Alisema kutokana na uchache wa sekondari  mkoani hapa kwa muda mrefu , kumekuwa nyuma kielimu ukilinganisha na mikoa mingine iliyoendelea kielimu hata hali ya ufaulu  ni wa hali ya juu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Kibondo, Daniel Makanga aliwataka wazazi kuwasimamia watoto wao na kutimiza wajibu wao kama walezi.

No comments: