WANANCHI wa Kijiji cha Munyegera wilayani Kasulu wamekataa kuchukua miili ya wananchi wawili wa kijiji hicho hadi watakapopewa maelezo ya kina ya sababu za kifo cha mmoja wao aliyekuwa mahabusi.
Akizungumza mjini hapa jana Mwenyekiti wa kijiji hicho, Tryphone Lilakoma alidai kuwa Desemba 3 mwaka huu polisi walivamia kijiji chao na kukamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu wawili waliouawa na kuchomwa moto Aprili mwaka huu.
Alidai kuwa mmoja wa waliokamatwa Tatizo Michael ambaye siku mbili baadaye polisi walitoa taarifa kwa ndugu zake kuwa mtuhumiwa huyo alifariki kutokana na maumivu akiwa mahabusu.
Kwa mujibu wa madai ya taarifa hizo, Michael alikuwa na maumivu yaliyosababishwa na kutumbukia kwenye shimo na kuumia siku aliyokamatwa wakati akikimbizwa na polisi.
Kutokana na taarifa hiyo, Lilakoma alidai kuwa wananchi wa kijiji hicho kwa hasira walivamia nyumba ya mmoja wa wanakijiji hao, Cosmas Chubwa na kumpiga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufa wakimtuhumu kuwaita polisi kijijini kukamata watu.
Diwani wa Kata ya Munyegera, Bungwa Dickson alidai kuwa matukio ya polisi kukamata watu kijijini na baadaye kukutwa wamekufa yamechangia kuwafanya wananchi kuwa na hasira na wametaka kuundwe tume ya kuchunguza kadhia hiyo ili polisi waliohusika wachukuliwe hatua.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraiser Kashai alidai kuwa Michael aliyekamatwa Desemba 3 mwaka huu kijijini hapo alifariki kutokana na maumivu aliyopata baada ya kudondoka kwenye shimo wakati akikimbizwa na polisi.
Kamanda Kashai alidai kuwa kutokana na maumivu hayo, kabla ya kuwekwa mahabusu Michael alipatiwa matibabu lakini akiwa mahabusi aliendelea kulalamika kuwa na maamivu.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kashai, Michael alifariki wakati wakijiandaa kumpeleka Hospitali ya Wilaya kwa mara ya pili baada ya hali yake kuanza kubadilika.
Akifafanua tukio zima, Kamanda Kashai alisema Aprili mwaka huu mfanyabiashara mmoja wa kijiji hicho alikutwa amechinjwa porini na taarifa zikaripotiwa polisi.
Alidai kuwa wakati polisi wakienda eneo la tukio walikuta wananchi wengine wawili wakiwa wameuawa kwa kuchomwa moto wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo ya awali.

No comments:
Post a Comment