Karibu kwenye Blog ya Kijamii ya Kigoma yetu kwa habari na matangazo kwa bei nafuu sana. Tunakalibisha maoni, ushauri na habari zako ili tuijenge Tanzania kwa pamoja.

Saturday, December 10, 2011

‘Ukusanyaji taarifa za Ukimwi ni tatizo’

Kuna changamoto kubwa katika kukusanyaji wa taarifa za watu wenye VVU wanouguzwa majumbani kutokana na kutokuwepo kwa mfumo rasmi wa kufanya shughuli kama hiyo.

Meneja Mradi wa Huduma za Wagonjwa Majumbani ulio chini ya kitengo cha Ukimwi cha Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKAIDS), Sudi Msumi alisema hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa watoa huduma majumbani kuhusu utoaji taarifa.


Alisema Mkoa wa Kigoma hauna utaratibu rasmi wa utoaji wa taarifa kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa na ndiyo maana inakuwa vigumu kupatikana kwa taarifa hizo.


Ili kuziba pengo hilo alisema kuwa BAKAIDS inaendesha semina ya siku tano kwa watoaji huduma majumbani, wasimamizi wa huduma majumbani katika zahanati na viongozi wa zahanati katika kata 12 za wilaya ya Kigoma zilizo chini ya mradi huo.


Msumi alisema kuwa baada ya mafunzo hayo watoa huduma hao wataweza kukusanya, kutunza kumbukumbu na kutuma taarifa za kile wanachofanya katika jamii kulingana na mfumo wa kiserikali kuanzia ngazi ya zahanati hadi taifa.


Akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uhusiano mema ya kidini mkoani Kigoma, Shaban Guoguo aliwataka watoa huduma majumbani kuwa na huruma, kutunza siri za wagonjwa na kuwajali wagonjwa wa Ukimwi kama sehemu ya familia zao.

No comments: